Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Friday, December 31, 2010

Apointiment

Dereva mmoja alikua akitafuta pa kupaki gari yake bila mafanikio,
Ikafika hatua akabandika kikaratasi kimeandikwa "nimezunguka jengo kwa dk 20 sijapata pa kuegesha gari. Hivyo nimeamua kuliegesha hapa nina apointment vinginevyo ntapoteza kazi yangu" akakiweka kwenye kioo na kukishikizia na wiper.

Aliporudi akakuta na yeye kikaratasi cha mkatisha ticket za parking kimeandikwa "nimefanya kazi hii kwa miaka 20 na hii ndio mara ya kwanza siwezi kukuachia vinginevyo ntapoteza kazi yangu"

No comments:

Post a Comment