Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Sunday, October 17, 2010

Ajali

Dereva mmoja alimgonga mwanamke mmoja barabarani. Wakati anaulizwa hali ikawa hivi:
Raia wa kawaida: Sasa hapa nani mwenye makosa?
Dereva akajibu: Mwanamke.
Raia: Kwa nini unasema mwanamke ndio ana makosa?
Dereva: Kwanini amekuja barabarani badala ya kuwa joikoni?

Mkate

Mteja: Habari? Nipatie mkate.
Dukani: Unataka upi? Mweupe au Wa brown?
Mteja: We nipe wowote nae mnunulia ni kipofu.

Mtoto na babu!

Mtoto alikua amekaa kibarazani na babu yake.
Mtoto: Babu nikuulize swali la kizushi?
Babu: Uliza mjukuu wangu.
Mtoto: Unaikumbuka siku ya kwanza uliyo-kiss?
Babu: Mjukuu wangu hiyo ya mwisho tu siikumbuki sembuse ya kwanza!!

Saturday, October 16, 2010

Miguu ya chura

Jamaa aliingia kwenye restaurant ya wachina akamuita mhudumu na kumuuliza, ''aisee una miguu ya chura?''
Mhudumu akajibu ''ndio mkuu''
Mteja: Okey basi ruka mara moja hapo mtaa wa pili ukanichukulie sigara tatu.

Toilet paper

Jamaa alienda nunua toilet paper, mkewa akamuuliza ''sasa mbona umenunua nyeupe tuu mi nilitaka za rangi?''
Mume akajibu: Za rangi ni gharama kidogo ntazipaka rangiz hizi hizi nyeupe usiwe na wasiwasi.

Watalii

Mtalii mmoja alitekwa bahati mbaya na watu porini asiowajua, akaulizwa ''what is your name?''
Mzungu yule mtalii akanena na yeye ''kwa nini mnataka kujua jina yangu?''
Mmoja wa watekaji akajibu ''ni kwa ajili ya menu ya leo''

Kuibiwa

Jamaa mmoja aliamka usiku mkubwa akaenda sebuleni kuchukua betri aweke kwenye tochi.
Alipoweka tu na kuwasha akakutana na kibaka ndani ya nyumba yake.
Kibaka: Nimekuja kukuibia kaa kimya...
Mwenye Nyumba: Oh! Okey mi nazima tochi naenda kulala ukipata kitu chenye thamani niamshe nkusaidie kubeba!

Mapenzi

Mwanamke akiwa dakika za mwisho hoi hospitalini akimuambia mumewe.
Mwanamke: Mume wangu niahidi utatafuta mwanamke mwingine nikifa.
Mwanaume: Nakuahidi mke wangu.
Mwanamke: Utampa jaketi langu alivae uwe unanikumbuka?
Mwanaume: Mhh! Mbona lile jacket halimtoshi ye mnene kidogo.

Kutoroka

Wafungwa wawili walipanga njama za kutoroka:
mfungwa wa kwanza: Tufanye hivi tukifika pale getini si kuna ukuta? Halafu tunapanda na kuruka.
Mfungwa wa pili: Anha! Tuchimbe chini kwa chini ndio.......!

Wakaamua wachukua choice one, walipofika eneo la geti kubwa mmoja kati yao akasema ''shenzi kumbe hamna ukuta!!''

Ugonjwa wa kusahau

Mwanamke: Dokta nimekuja nna tatizo, mume wangu ana tatizo la kusahau sana.
Dokta: Ooh! Nini dalili za hilo tatizo alilo nalo?
Mwanamke: Akiona mwanamke mzuri tu anasahau kua ameshaoa!

Kununua maua

Jamaa mmoja alikua akienda duka la maua kila siku ya ijumaa kununua ua/maua!
Muuza maua: Unayapenda maua yetu eenhe?
Alimuuliza jamaa kwa ujio wake.
Jamaa: Hii ndio mara ya mwisho nanunua maua hapa.
Muuzaji: Kwa nini tena?
Jamaa: Kwa sababu kuanzia kesho ntakua nimeshaoa!

Hii tamu

Jamaa mkewe alijifungua mapacha!
Jamaa: Ebwana mke wangu si kajifungua mapacha bwana!
Rafiki: Mbona jambo la kawaida ndugu yangu.
Jamaa: La kawaida ndio lakini swali sijajua yule pacha mwingine ni mtoto wa nani?

Thursday, October 14, 2010

Jani

Mtoto mmoja alienda na mama yake kwenye makumbusho ya picha na sanamu mbalimbali. Punde akaona Sanamu moja ikiwa uchi kasoro sehemu nyeti ikiwa imefunikwa na jani la sanamu na lenyewe, mama yake akamuuliza ''mbona hautokia hapo?''

Mtoto akajibu, ''nasubiri hili jani lianguke''

Kuku wadogo

Dogo mmoja alienda restaurant na kuagize kuku!
Akamuambia mhudumu ''aisee nletee kuku sio mkubwa mwili wangu sio mkubwa, nataka kuku mdogo tuu''

Mhudumu akaenda andaa mlo na alipomletea akamletea mayai mawili kwa kigezo cha kuku wadogo.

Wednesday, October 13, 2010

Vichaa watatu

Vichaa watatu walitoroka hospitali ya vichaa:
Wakaanxa ulizana wakati wapo nje
Wa kwamza: Eti saa hizi mchana au usiku
Wa pili: Itakuwa usiku kwani lile jua au mwezi?
Wakamuuliza mwenzao ''eti we unaonaje maswali yetu?''
Akawajibu ''mie sio mwenyeji hapa''

Tuesday, October 12, 2010

Kupima macho

Jamaa mmojaalienda kupima macho, wakati yupo kwa daktari akavishwa lenzi ili aweze kusoma maandishi madogo yaliopo kwenye ubao:

Dokta: Haya soma haya maandishi yaliyopo kwenye huu ubao.
Mgonjwa: Ubao gani dokta?

Mzigo umevuka

Kulikuwa na jamaa mmoja alikuwa tall kweli kweli kiasi kwamba vitanda vya shule ya bording miguu inavuka kitanda.

Siku moja wanafunzi wenzake wakamfunga kitambaa chekundu miguuni eti mzigo umevuka body ya gari/lori. (mithili ya lori inavyokuwaga).

Sunday, October 10, 2010

Volks Wagen

Mama mmoja alisimamishwa na traffic police kwa kosa la kupita njia ambayo hairuhusiwi akiwa na gari aina ya Volks Wagen (mgongo wa chura) akajibu, ''traffic jaman gari lenyewe dogo halijui kitu''

Riadha

Daah! Aisee nimekimbia mita 500 kwa sekunde thelathini. Jamaa mmoja akimuambia mwenzake. Mwenzake nae akamjibu ''haiwezekani kwani hata mwanariadha wa dunia hawezi hiyo kitu''

Jamaa akamjibu: Si nimegumdua shortcut way.

Friday, October 8, 2010

Mboga

Wasukuma walienda kumtembelea mkwe wao, wakaletewa viazi nyama. Maongezi yao yakawa hivi:
Msukuma wa kwanza: Tumeenda kwa mke wa K si akaturetea mboga tupu.
Jamaa anaesimuliwa akanena: Kwa nini?
Msukuma akajibu: Si hatukuona ugari.

Kitambi

Mtoto akimuuliza mama yake, ''mama... mama... Kwani mimba ya baba nani kampa?''
Akimaanisha kitambi.

Thursday, October 7, 2010

Hii nayo...

Mtoto: Mama eti mtoto anazaliwa pale baba anapoingizaga dudu yake.
Mama: Ndio mwanangu.
Mtoto wa kike mae akadakia, ''sasa meno je hawezi yang'oa kweli?''

Kaka na Dada

Kaka ma dada wakiangalia tv, kaka akawa ma hamu ya kufanya mapenzi akamuambia dada yake.
Dada akajibu, ''wewe mi si dada yako?''
Kaka akanena, ''so what?''

Kaka akazidi bembeleza mpaka waka-do.
Walipomaliza kaka akamuuliza vipi ume-enjoy?
Dada akajibu ''sio tamu kama nikiwa na babu yeye zaidi''

Sukuma gari

Mtoto: Mama kwa nini tunaisukuma gari ya baba tu tuwashe tuondoke.
Mama: Shhh... Utamuamsha baba yako.

Tuesday, October 5, 2010

Annivessary

Mume alimnunulia tiket ya ndege kwenda Peru siku yao ya annivessary, mke akamuuliza mumewe ''enhe mume wangu annivessary ijayo utaninunulia nini?''

Mume nae akamjibu: Ntakununulia ticket ya kurudi (return ticket).

Pombe bwana

Jamaa mmoja alirudi kwake, alipofika sebuleni akawa analigonga gonga lile bwawa dogo la kioo la kufugia samaki. Mkewe akamuuliza ''unafanya niniz?'' Jamaa akajibu ''nawazuia hawa samaki wasinibwakie (kama mbwa)''

Sunday, October 3, 2010

Kumuona daktari

Jamaa alienda zahanati moja alikuwa anaumwa, akaambiwa kumuona daktari ni shilingi elfu mbili.
Jamaa akadakia na kujibu ''sina hiyo elfu mbili ntafumba macho nsimuone ili insilipe.

Friday, October 1, 2010

Wizi

Mama mmoja aliambiwa mwanae ameuwawa kwa sababu ya wizi akajibu hivi, "maskini Tarimo alikua anafanya kazi ya ujambazi akiniletea pesa za kuishi, sasa hiyo kazi ya wizi ameanza lini tena?"

Kipofu

Jamaa mmoja alikuwa amekaa sehemu na rafiki yake kipofu, sasa wakati wanatwanga stories yule kipofu akamuuliza mwenzake asiye kipofu, "hivi umeiona movie mpya ya Kanumba? Aisee kali acha."

Godoro

Jamaa alikua anamfukuza mtu alietoka na godora lake kwake. Mfukuzwaji alipoona jamaa bado anamfukuza akaingia kituo cha polisi.
Polisi: Wewe vipi na godoro?
Jamaa: Kuna mtu ananifukuza mi mwizi wake.

Mwenye godoro akafika, "samahani polisi huyu ni ndugu yangu ana matatizo ya akili kidogo naomba niondoke nae tafadhali."

Jamaa: Hapana jamani mimi mwizi wake nimemuibia hili godoro.....