Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Wednesday, December 21, 2011

Mbele ya kioo Part ii

Katoto ka miaka minne kalifuatwa na kuulizwa "wewe kusinzia mbele ya kioo kulikoni na unachelewa mafundisho?"

Dogo akamjibu baba ake "baba mie melala hapa ili ukifika muda mwenzangu kwenye kioo aniamshe kumbe na yeye kalala pia."

Mbele ya kioo

Mama mmoja alimkuta mwanae amelala huku akiwa,mbele ya kioo cha kujitazama. Mama akamuuilza "we Esther mbona umelala mbele ya kioo vipi?"

Mtoto nae bila hiyana toka usingizini akajibu "si nimelala hapa ili nijione nkiwa nimelala"
Akasisitiza "yaani nijue kweli nimelala au nipo macho."

Tuesday, December 20, 2011

Maskini kipato

Mama: Mwanangu mbona upo na huzunika sana.
Mtoto: Majirani zetu inaonekana maskini sana, mtoto wao kameza 100Tsh tu wamechanganyikiwa je angemeza elfu 10?

Saturday, December 17, 2011

Kiingereza

Jamaa mmoja wakati anapita sehemu alisikia mtu akiongea lugha ya kigeni kiinglishi. Papo hapo akanena kimya kimya akanena (kwa vile kizungu akichoongea ilikua kimobomoka bomoka mno)

"mmh huyu jamaa anaongea lugha inayofanana na kiingereza"

Friday, December 16, 2011

Hii kali

Mwanamke katikati ya ndoto akiweweseka "ondoka fasta fasta mume wangu amerudi" jamaa alie pembeni yake akatoka nje na nguo zake kujificha. Alipofika nje akagundua kuwa aliekua anaota ni mkewe na yeye alilala nyumbani kwake pia.

Walevi wawili.

Mlevi: Jana mke wangu alikua kwenye Tv
Mlevi 2: Aliingiaje sasa?
Mlevi 1: Sijui alichukua stuli maana Tv ipo ukutani.

Kengele

Mwenye nyumba wakati anatoka akakutana na mtu "wewe ni nani?" Jamaa akajibu "fundi wa kengele,nimekuja rengeneza"

Mwenye nyumba "sasa si ungekuja tangu jana fundi?"
Fundi "nipo mlangoni tangu jana nabonyeza tu kengele hamna anaekuja kufungua mlango"

Kituo cha polisi

Kijana alipofika kituo cha polisi.
Kijana: Nimekuja uliza, hao kwenye picha ukutani ni akina nani?
Polisi: Hawa watuhumiwa sugu wanatafutwa na polisi.
Kijana: Khaa! Nyie wazembe sa si mngewakamata wakati mnawapiga izo picha!?

Fundi kitandani

Mwanamke akimuambia fundi "bora umekuja yaani treni ikipita tu nje nyumba inatetema nusula nidongoke toka kitandani" akamuambia fundi apande kitandani ashuhudie mwenyewe.

Wakati fundi yupo kitandani mume akaingia "haya nini maana ya hii hali fundi yupo na wewe chumbani?"
Mke akajibu "utaamini kuwa alikua anaisubiria treni?"

Kilo mbili

Jamaa alienda kujiunga jeshi la polisi, alizidi kilo mbili akakataliwa. Akaenda saluni kunyoavna aliporudi kupima mzani akakutwa bado kilo moja.

Dogo akamjibu afande "afande hii kilo moja iliyobaki kupungua itapungua nkioga na kukojoa tu"

Wednesday, December 14, 2011

Matokeo mtihani

Dogo alipata 90 kwenye pepa. Mshua alipoona akamuambia "mwanangu sa si ungepata 100 kabisa"
Dogo akajibu "tatizo Juma aliandika mwandiko mbaya jibu la mwisho sikuona vizuri"

Joto

Abiria: Konda ondoeni gari bwana joto humu...
Konda: Oya usituzengue, shuka kapande friji.

Tuesday, December 13, 2011

Siti zipo

Abiria: Siti zipo humo ndani au imejaa?
Konda: We chizi nini kwani umesikia wamekalia ndoo humu ndani?

Hamnazo

Baba baada ya kupekua daftari za mwanae "wewe mbona madaftari yapo matupu?"
Mtoto: Niliandika labda nlisahau kupiga mistari maandishi yatakua yamedondokea kwenye begi.

Vioja daladala

Konda: Oya kamatia gari inaondoka hii...
Abiria: Siti zote zimejaa ivo ntakaa wapi?
Konda: Usinizengue, km vipi ungekuja na siti yako.

Monday, December 12, 2011

Swali kwa padre

Kijana akimuuliza padre "fatha nauliza, hivi peponi kuna futball pia?"
Padre: Njoo kesho tafadhali ntakua nimepata jibu.
Siku ilofuata akaja.
Padre akajibu "...ndio kuna futball na una mechi ya kucheza alhamis hii"

Kwa wakili

Wakili: Inakuwaje unataka talaka kumpa mkeo mzuri kiasi hiki?
Mume: Ona kiatu changu kilivyo kizuri, lakini mvaaji pekee ndio anajua kiasi gani kinambana.

Nani kabla ya ndoa

Mwanaume: Nilikua Milionea kabla sijaoa.
Rafiki: Safi, sasa ivi si ndo mnahela zaidi?
Mwanaume: Hapana nilikua bilionea hapo awali.

Kwenye treni

Mkaguzi tiketi kwenye treni "vipi mzee mbona hofu? Usiogope mzee wangu hamna shida ya kukufanya uogope."
Mzee nae akajibu "ohh afadhali maana nimepanda na sijakata tiketi ya safari yangu."

Sunday, December 11, 2011

Kwenye daladala

Mlokole mmoja alipanda Daladala moja
ambayo ulikuwa inatwanga mziki Wa kidunia
kwa kwenda mbele,Mlokole: nyimbo gani mnapiga hizo, wekeni nyimbo
za Yesu"Kond a akamjibu... ..."Yesu bado
hajatoa albamu.... .."

Saturday, December 10, 2011

Dereva wa daladala

Dereva wa daladala alisimamisha basi akampisha bi.mkubwa mmoja kwenye kiti chake. Abiria wakauliza "dereva vipi nani ataendesha sasa?"
Dereva akajibu "mpaka mtu ajitolee mpisha bibi huyu ndio ntarudi kwenye kiti changu"

Kung'oa jino

Dokta meno: Ajabu kweli nimeng'oa meno matatu ya mbele hata damu haitoki!!
Mgonjwa: Aahh umeng'oa ya bandia sio yenyewe.

Kwa dokta

Dokta: Hizi dawa ili mumeo apate usingizi.
Mke: Ohh atakiwa ameze saa ngapi?
Dokta: Ni zako wewe ukameze sio yeye.

Wednesday, December 7, 2011

Kibweka kanisani

Jamaa mmoja alikua anampenda sana dada mmoja. Akamfuata mpaka kanisani, ilipofika wakati wa kutoa sadaka jamaa akamuwahi dada na kumuambia "ohh kuhusu sadaka acha tu ntakutolea"

Baada ya mtihani

Baada ya kutoka chumba cha mtihani, wanafunzi walikamatana na kudundana mingumi ya kutosha. Mwalimu alipowakuta na kuwauliza kwanini wanapigana, mmoja wao akajibu; 
"mwalimu mimi mtihani wa hesabu sijajibu kitu, nimeandika jina tu, sasa huyu b.w.e. g.e nazi naye kaniiga, hajajaza kitu, ameandika jina tu sasa si itaonekana mmoja wetu amekopi kwa mwenzie halafu tutafutiwa matokeo wote!"

Sunday, December 4, 2011

Kichaa kapewa rungu

Kijana alikua anafukuzwa na kichaa aliekua na rungu mkononi kwa umbali wa kilomita 1. Alipochoka akaamua kusimama. Kichaa alipomfikia akam-dalika kidali poo kisha akamuambia "kalale nacho"

Kibweka kitandani

mzee mmoja alikuwa amelala na mkewe,akawa
anajamba kwa sauti mbali mbali,mkewe ikabidi
amuulize kulikoni mume wangu? mzee
akajibu"Potezea bna,Natafuta ringtone ya
matako yangu!"

Friday, December 2, 2011

Somea mtihani

Madogo wawili wa shule ya msingi:
Dogo A: Mtihani keshokutwa sa tunafanyaje?
Dogo B: Kuchemsha daftari tu na kunywa maji.
Dogo A: Tatizo notice zangu nyingi tashindwa maliza hayo maji.

Msiba wa kipenzi

Mwanamke mmoja alifiwa na mumewe kipenzi, siku ya mazishi akaomba msaada mmoja akisema "naombeni mumzike na hii simu yake na chaja niwe nawasiliana nae." Kisha akakumbuka jambo "aahh umeme wa kuchajia hata kuwa nao."

Thursday, December 1, 2011

Mtoto wa nani?

Mtoto alizaliwa na tangu azaliwe hakuwahi ongea. Kwa mara ya kwanza siku akataja "bibi" siku moja mbele bibi ake akafa.

Akataja tena baada ya miezi "babu" ikawa vilevile. Miezi tena akataja "baba" ndipo baba alipoanza andika urithi nk. Kilichofuata akafariki dereva wao.