Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Saturday, August 21, 2010

Vekesheni

Jamaa alienda vekeshe na mkewe. Bahati mbaya akafia wakati wapo vekesheni Jerusalem.

Akaambiwa kumsafirisha mpaka nchini mwao ni dola 3000, wakimzika Jerusalem ni dola 300 tu.

Jamaa akakataa kumzika pale pa dola 300 huku akisema "hapo zamani sana alikufa akafufuka baadae, mi sipo tayari mke wangu afufuke."

Kibosile akifa

Boss mmoja hospitalini hoi kitandani, alimuita mwanasheria wake, daktari na mchungaji.
Akawaambia "hapa nna dola elfu90 chini ya mto. Nimeziweka kwenye bahasha dola elfu 30 tatu. Nataka nikifa kabla hawajatupia udongu mzirushie kaburini."

Wakaitikia "sawa, haina shida"

Baada ya mazishi:
Mchungaji: Acha niseme ukweli nimechukua dola elfu10 tu kwa ajili ya ujezi wa kanisa ingine kama marehemu alivyoagiza.

Dokta: Mie nimechukua dola elfu15 tu ingine kama marehemu alivyosema.

Mwanasheria: Mie niliziweka kwenye akaunti yangu, nikaandika cheque na kuiweka kwenye bahasha nkafanya kama marehemu alivyosema...

Za nyuma

Unaikumbuka hii?
Nyoka m1 asked the atha "ivi sisi tuna sumu?" Mwenzake akajibu "ndio, why?" AKAMJIBU "nimejing'ata bahati mbaya!"

Ndio|Hapana

Kwenye mtihani wenye majibu Ndio|Hapana
Msimamizi mmoja alimfuata mwanafunzi wakati anasimamia mtihani akamuuliza "mbona unarusha rusha hiyo sarafu ya sh 100?"
M'funzi: Nahakiki kama majibu nlojaza ni sahii.

Mboga za majani

Mama mwenye nyumba aliporudi akauliza "mbona sebule ipo hivi leo?"
House girl akajibu "nimesahau kupanga vizuri, nilichukua hiyo mboga ndo naipika"
Mama akanena "weewe!! Hayo uliochukua ni urembo sio majani halisi (artificial mimea)

Akon

Unaujue wimbo wa AKON "lonely" basi nausikiliza hapa, AKON anauimba kanyong'onyeaa sijui "swaumu imemkolea?"

Kipindi cha tv

Mtoto mmoja wakati anaangalia kipindi kizuri kwenye televisheni akamuita mama yake "mama... mama njoo haraka uone"

Bahati mbaya mama yake akakosa hiyo sehemu, mwanae akasema "aaahh umecheleewa"

Mama nae akajibu "tv ya chumbani si unajua ipo dakika 4 nyuma itakuwa haijaonyesha ngoja nikaangalizie huko."

Ndoto tatu

Vijana watatu wakisimuliana ndoto ya jana usiku:
Wa 1: Aisee jana nimeota namiliki BMW new model.
Wa 2: Mie ndo funika, nimeota namiliki PPF Tower.
Wa 3: Mie yangu jana si nimeota namiliki wake zenu.

Mke na mume

Mwanamke mmoja alimpigia simu mumewe akiwa mbali nae.
M'ke: Umeamkaje m'me wangu?
M'me: Nimeamka na hang-ova leo mpenzi wangu.
M'ke: (kwa ukali alisema) nilijua tu nikisafiri utamleta tena huyo mwanamke wako.

Toto tundu ii

Mama mmoja wakati anamfokea mwanae mdogo alieharibu jambo alimalizia kwa kumuambia...
"...muone kwanza, sura mfuko wa jeans"
Mtoto akauliza "wa mbele, wa nyuma?"

Toto tundu

Mtoto mmoja alikua anaitwa Happy, na dada wa kazi za ndani nae anaitwa Happy. Sasa siku moja mama yake mtoto akamuambia mwanae Happy amuite dada aje...

Kwa vile alikuwa mbali kidogo yule mtoto ilimbidi aite kwa sauti kubwa kidogo "H.a.p.p.y!... Haaappy..." kituko ni pale alipokua akiita na yeye muitaji anaitika.

Mama yake akamuuliza "sasa mbona unaitika we mwenyewe tena?"
Mtoto akajibu "kwani na mimi si jina langu Happy?"

Friday, August 20, 2010

Mtoto kupotea

Mtoto mmoja alipoteana na dad yake mlimani city. Akakutana na askari akamuambia "nimepoteana na baba yangu namtafuta"

Askari akauliza "huwa anapenda nini haswa?"
Mtoto akajibu "bia na wanawake wenye nyonyo kubwa"

Pampus

Mtoto mmoja wakati anavishwa pampus huku baba wa toto akiwa pembeni.
Alikuwa anaangalia mwanae akivishwa pampus akamuuliza mkewe "hivi hizo kitu (pampus) huwa zina mifuko?"

Mke anapaki

Jamaa alirudi nyumbani akakuta mkewe anapakia nguo kwenye begi lake la safari.

Mume akauliza, "unapaki nguo unaenda wapi mke wangu?"
Mke akajibu, "naenda Daslam, nasikia wanawalipa dola 300 malaya. Bora niende huko kuliko kukupa tu bure."

Mchumba

Katoto kamoja siku moja alimuuliza bibi yake wa miaka 94.
"bibi... kwani we kuna mchumba?"

Bibi akajibu "mjukuu wangu, mchumba wangu ni tv, ndio anaenipa furaha na kuniondolea mawazo"

Sasa siku moja tv ilikuwa inaonyesha chenga chenga... Bibi akawa anaipiga piga/gonga gonga ionyeshe vizuri.

Kidogo mtoto akasikia mlango unagongwa akaenda fungua.
Kumbe alikuwa mchungaji kaja kumuona bibi.

Mchungaji: Hujambo...? Bibi yupo?
Mtoto: Yupo chumbani anampet pet mchumba wake.

Kupima damu

Mtoto mmoja alimkuta rafiki yake hospitali analia, akamuuliza "unalia nini?"
Dogo mwenzake akajibu "nimekuja kupima damu wamenikata kidole.''

Rafiki yake nae akaanza kulia. Mwenzake aliekuja kupima damu akamuuliza "unalia nini sasa na wewe?"
Mwenzake akajibu "mi nimekuja kupima mkojo"

Mgonjwa kwa dokta

Mgonjwa: Dokta nimekuja unibadilishie dawa.
Dokta: Dawa? Kivipi? Sijaelewa.
Mgonjwa: Mi naumwa kichwa ila dawa uliyonipa mbona nikimeza inaenda tumboni badala ya kichwani?

Naomba maji

Mtoto mmoja alipoenda kulala mara ghafla akaita... ''baabaa... naomba maji ya kunywa"

Baba akajibu, "lala bwana utakojoa kitandani."

Dakika chache baadae mtoto akasema vile vile tena. Baba nae akajibu vilele.

Awamu ya tatu mtoto akaomba tena na baba akajibu "sasa ntakuja na kiboko nikuchape, mbona hunielewi"
Mtoto akajibu "baba ukija na hiyo fimbo njoo na maji ya kunywa"

Kuchora mbwa

Kwenye kipindi cha sanaa wanafunzi waliambiwa wachore mbwa kafungwa kamba...

Baada ya muda mtoto mmoja akawa anatoka nje. Mwalimu akamuuliza "wapi unaenda?"
Mwanafunzi akajibu "namtafuta mbwa imebaki kamba tu nliyoichora, itakuwa amekata"

Bunduki

Jamaa alinunua bunduki, majaribio akam-shoot mwanae.
Alipokufa akasema ''aanha kumbe sio ya kichina"

Hii kutoka kwa...

Kichekesho hiki nlikisoma siku nyingi toka kwa cartoonist fadhil (jina la pili limenitoka)

Jamaa alienda kwa daktari wake alipofika akamuuliza dokta wake ''dokta! Hivi ile dawa ya kupaka uliniambia ninywe mara ngapi?"

Kuibiwa simu

Jamaa mmoja aliibiwa simu, sasa wakati anabishana ''simu yangu simu yangu.." akasema "kama unabisha tukapime DNA.

Thursday, August 19, 2010

Kupata mtoto

Katoto kamoja ka kike kalinyoosha mkono darasani kakauliza;
Mtoto: Mwalimu, bibi yangu anaweza kupata mtoto?
Mwalimu: Hapana ni mzee sana, hawezi.

Mtoto: Mama yangu je?
Mwalimu: Anaweza kupata, lakina na yeye amefikia uzee pia.
Mtoto: Mimi je?
Mwalimu: Ee! Hapana huwezi bado mdogo sana kupata mtoto.

Kavulana kamoja kakadakia na kusema mbele ya darasa zima ''unaonaa? Mi nlikuambia usiogope''

Nikifa

Jamaa alitishiwa kisu wakati wanataniana na rafiki yake, alietishiwa kisu wakati wa utani huo akasema ''weuwe, ooh, shauri yako. Nikifa utanitambua.''

Maelekezo

Jamaa akimuelekeza dereva aliekuwa nae vijijini wakati wa kuvuka daraja la kienyeji la magogo.

Kilichokua kinatakiwa kufanyika ni amuelekeze dereva akanyage kulenga magogo ili isije ikatelezea mtoni.

Mwongozaji akawa anamuelekeza ''njoo njoo njoo..." huku eti mkono mmoja kajiziba uso kwa uoga wa kushuhudia.

True story

Kuna siku wakati wa mizunguko ya ukaguzi vijijini tulifika kijiji kimoja, wananchi wawili watatu katika nyumba moja walitoka nje haraka haraka wakidhani askari. Kisa cha yote kwenye kijumba hiko kinauza podbe haramu ya Gongo.

Wednesday, August 18, 2010

Ujiko

Kijana mmoja wa makamo aliopoa mrembo. Sasa wakati wapo evening walk alipoona gari aina ya prado inakuja kwa mbele akajirusha mbio kwenye kichaka.

Yule mrembo akamshangaa na kujiuliza. Akamuuliza ''vipi?''
Kijana akajibu, ''umeiona ile prado?''
Dada akajibu ''ndio'' kaka akaendelea ''ni ya nyumbani ile sijui baba yule?''

Maongezi yalipoisha jamaa akamuambia yule mrembo ''samahani nisaidie kutoka miba zimezidi nikamata''

Kiti

Baba mmoja alipata wageni kwake nyumbani. Akamtuma mwanae aongeze viti pale sebuleni.

Mtoto kwa vile ilikuwa hamna namna tena ya kupata kiti kimoja cha ziada, akaenda kung'oa kiti kimoja toka kwenye gari ya baba yake.

Alipoulizwa na baba yake amekitoa wapi akajibu ''nimekiazima kwa jirani baba''
Baba akajibu ''ooh kumbe, kizuri, usikirudishe tutamuambia kiliibiwa.''

Kesho yake baba kutoka nje akaona gari yake haina kiti akaanza kufoka, mtoto akadakia "baba ni hivi jirani aliona nachelewa kurudisha akachukua cha gari yako, sasa wewe mkomeshe chukua hiki ufunge kwako."

Simenti

Jamaa mmoja alijikuta anakanyaka ciment. Na alikuwa amelewa. Alipofika nyumbani akalala hivyo hivyo na viatu.

Asubuhi alipoamka akakuta mwanae anamwagia maji miguuni ''wewe unafanya nini?'' aliuliza kwa ukali.

Mtoto akajibu ''mama kaniambia nimwagie maji ciment ishike vyema usiende kulewa.''

Nusu kwa nusu

Bibi na babu walienda best bite, wakaagiza burger moja babu akaanza ikata nusu ampatie bibi.

Kijana mmoja alikuwa akiwaangalia akawauliza "niwanunulie ingine?"
Babu akajibu ''hapana hii tutagawana nusu kwa nusu.''

Kijana akamuuliza bibi "bibi na wewe utaanza ila?''
Bibi akajibu ''nasubiri kwanza, sasa hivi ni zamu yake kutumia meno yetu.''
(sijui ya bandia...?)