Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Friday, August 20, 2010

Mchumba

Katoto kamoja siku moja alimuuliza bibi yake wa miaka 94.
"bibi... kwani we kuna mchumba?"

Bibi akajibu "mjukuu wangu, mchumba wangu ni tv, ndio anaenipa furaha na kuniondolea mawazo"

Sasa siku moja tv ilikuwa inaonyesha chenga chenga... Bibi akawa anaipiga piga/gonga gonga ionyeshe vizuri.

Kidogo mtoto akasikia mlango unagongwa akaenda fungua.
Kumbe alikuwa mchungaji kaja kumuona bibi.

Mchungaji: Hujambo...? Bibi yupo?
Mtoto: Yupo chumbani anampet pet mchumba wake.

No comments:

Post a Comment