Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Saturday, August 21, 2010

Mwizi|Mwalimu|M'sheria

Mwizi, Mwalimu na Mwanasheria wote walikufa ghafla kwenye ajali mbaya.

Walipofika peponi wakaambiwa nako kumejaa ila atakaepatia jibu la swali ndio ataingia...

Mwalimu aliulizwa "ni meli gani ilizama Tanzania?" akajibu MV. Bukoba.
Akaambiwa amepatia aingie.

Mwizi akaulizwa "ni watu wangapi walipoteza maisha kwenye hiyo ajali?" mwizi akajibu 150.
Akaambiwa amepatia na aingie.

Mwanasheria akaambiwa kulingana na jibu alilotoa mwizi "wataje majina?"

No comments:

Post a Comment