Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Wednesday, August 18, 2010

Kiti

Baba mmoja alipata wageni kwake nyumbani. Akamtuma mwanae aongeze viti pale sebuleni.

Mtoto kwa vile ilikuwa hamna namna tena ya kupata kiti kimoja cha ziada, akaenda kung'oa kiti kimoja toka kwenye gari ya baba yake.

Alipoulizwa na baba yake amekitoa wapi akajibu ''nimekiazima kwa jirani baba''
Baba akajibu ''ooh kumbe, kizuri, usikirudishe tutamuambia kiliibiwa.''

Kesho yake baba kutoka nje akaona gari yake haina kiti akaanza kufoka, mtoto akadakia "baba ni hivi jirani aliona nachelewa kurudisha akachukua cha gari yako, sasa wewe mkomeshe chukua hiki ufunge kwako."

No comments:

Post a Comment