Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Thursday, August 19, 2010

Kupata mtoto

Katoto kamoja ka kike kalinyoosha mkono darasani kakauliza;
Mtoto: Mwalimu, bibi yangu anaweza kupata mtoto?
Mwalimu: Hapana ni mzee sana, hawezi.

Mtoto: Mama yangu je?
Mwalimu: Anaweza kupata, lakina na yeye amefikia uzee pia.
Mtoto: Mimi je?
Mwalimu: Ee! Hapana huwezi bado mdogo sana kupata mtoto.

Kavulana kamoja kakadakia na kusema mbele ya darasa zima ''unaonaa? Mi nlikuambia usiogope''

No comments:

Post a Comment