Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Saturday, July 31, 2010

Alarm

Kuna jamaa mmoja alipoisikia alarm ya gari fulani inapiga kelele, akawa anatembea huku akipepesha mikono yake juu kama kwaya masta anapoongoza nyimbo fulani ya kwaya.

Vizee

Kulikuwa na vibibi viwili vizee wakiongea, mmoja akamuambia mwenzake "siku hizi nnasahau sana, jana nilisimama kwenye ngazi nikawa sikumbiki kama nilikuwa nataka kushuka au kupanda?"

Wa pili nae akamuambia mwenzake, "mimi nilikaa kwenye kitanda nkawa sikumbuki kama nataka kulala au ndio nimeamka"

Wa tatu akawaambia wenzake, "Loh, mimi ndio sijielewei kabisa, juzi nilikuwa bafuni na ndoo ya maji nikawa sikumbuki kuwa ndio nataka kuoga au ndio nimemaliza tayari"

Friday, July 30, 2010

Besdei

Vizee viwili mke na mume siku moja wakati wapo mezani, mke akamuambia muwewe.
''tutoe nguo zote tule chakula bila kubanwa banwa.

Wakati wanakula mke akalalamika ''mh! nimeanza sikia joto ghafla.''
Ndipo mume akajibu ''ni kwa sababu titi zipo kwenye bakuli la supu.''

Thursday, July 29, 2010

Siku ya harusi

Mwanaume mmoja alikuwa na ugonjwa wa kusahau sahau sana, siku moja wakati yupo nyumbani anafua nguo zake na usafi kwa ujumla, ghafla akaingia mwanamke akiwa amefyumu ile mbaya. Kumbe alikuwa ni bibi harusi ndani ya vazi lake tayari, na huyo aliemkuta akifanya usafi ndio mume mtarajiwa, hakuonekana kanisani.

Uelewa huu?

Jamaa mmoja alipofika maeneo fulani fulani ya uzunguni akakuta kibao kimeandikwa "Amri hairuhusiwi kutembea eneo hili" yule kaka pamoja si akaamua kutambaa mpaka alipolimaliza hilo eneo...

Ndege pori

Eti wale ndege pori wanaopenda kula mizoga baada ya simbana wengineo kumaliza kula, na wao walipata kamzoga mpaka mwisho wa siku wakatosheka na kuwepo tu pembeni palipo huo mzoga. Ndipo akaja ndege mwenzao na wakamuambia "usitulaumu kuchelewa kwako, sie tushakula ukikikuta cha baridi hilo halitu-husu"

Shoga

Shoga mmoja mwanajeshi wakati yupo vitani akawa anabishana na mwanajeshi mwenzake, "we vipi unazubaa zubaa nini m-shoot huyo adui anazidi kuja karibu yetu?"
Ndipo yule shoga akamjibu "we humuoni alivyo mzuri vile, mi siwezi"

Kwa dokta

Mama mmoja aliporudi nyumbani akawa anaongea mawili matatu na mumewe, kidogo anaingia mtoto wao wa kike. Wakamuuliza "enhe za hospitali? Daktari anasemaje?"
Mtoto kwa nafasi nae akawa anajibu, "majibu mazuri tu, ila nimesahau chupi yangu kwa dokta" wazazi walitizamana...

Kwenye computer

Kibosile mmoja alimpigia secretary wake simu "mbona hujanijibu e-mail yangu mpaka sasa?"
Secretary akajibu, "boss nimeisoma ila nimeshindwa kuijibu, nipo nyumbani bado na kibaya ni kwamba paka wangu ameimeza "mouse"

Tembo

Kijana mmoja alikuwa na tembo wake mdogo akimfuga, siku moja wakati wapo matembezini jamaa akafungua zipu yake na kujisaidia haja ndogo, nipo tembo wake akamuuliza "unawezaje kupumua na huo mkonga wako?"

Harusi

Siku ya harusi bibi harusi alipofika kanisani akiwa ameshavalia gauni la harusi nk, kidogo anamuona mumewe mtarajiwa anatoka na bibi harusi mwingine amevaa kama yeye wakiwa tayari wamefunga ndoa. Bibi harusi wa kwanza akabaki kwenye mshangao asielewe kinachoendelea, ndipo mumewe mtarajiwa akamuuliza huyu wa awali, "Hukupata e-mail yangu?"

Simu haionekani

Mwanaume mmoja siku moja wakati yupo kwake ghafla akawa anasikia simu inaita halafu haioni, akaanza mlaumu mkewe " muone kwanza ushaificha simu yangu, mbona siioni na inaita?"

Mke akamuangalia na kumjibu; "una uhakika?"
Mume: Ndio
Mke akaenda akamfunua kitambi jamaa akaiona simu imejificha katikati ya nyama.
Mume akawa mdogo kama amemwagiwa maji ya baridi.

Wednesday, July 28, 2010

Mtoto huyu

Mtoto wa miaka 6 wa kike alienda sebuleni alipomkuta mama yake ameketi na baba yake.

Akasema, ''baba kondom yangu imepasuka una ingine ya akiba?'' mtoto alinena.
Mama nae kimoyo moyo akanena (mungu wangu mtoto huyu ameanza lini?)

Mama akauliza vizuri, ''imepasuka!? Umeipata wapi?''
Mtoto: Meipata kwenye suruali ya baba, nilikua naichezea...

Tuesday, July 27, 2010

Pancha

Baba mmoja alimuacha mwanae kwenye gari kwa muda. Punde kidogo mtoto akasikia kama gari inatikisika, kuchungulia akamuona kibaka ameinama kwenye tairi.

Mtoto akamuuliza yule kibaka, ''unafanya nini kwenye gari ya baba?''
Kibaka kujihami akajibu, ''baba yako kanituma nije kuziba pancha.'' Mtoto akasema 'oh okey'

Baba aliporudi akauliza, ''imekuwaje hamna matairi?'' mtoto ndipo akajibu, 'alikuja mtu akasema anaenda kuziba pancha ndo nkamuambia achukue yote manne akazibe asichelewe sana.''

Pancha

Baba mmoja alimuacha mwanae kwenye gari kwa muda. Punde kidogo mtoto akasikia kama gari inatikisika, kuchungulia akamuona kibaka ameinama kwenye tairi.

Mtoto akamuuliza yule kibaka, ''unafanya nini kwenye gari ya baba?''
Kibaka kujihami akajibu, ''baba yako kanituma nije kuziba pancha.'' Mtoto akasema 'oh okey'

Baba aliporudi akauliza, ''imekuwaje hamna matairi?'' mtoto ndipo akajibu, 'alikuja mtu akasema anaenda kuziba pancha ndo nkamuambia achukue yote manne akazibe asichelewe sana.''

Iki...

Mtoto mmoja alikua akimsikia baba yake usiku mara kwa mara akimwambia mama yake, ''ikisimama panda''

Siku moja akamuuliza mama yake, ''mama humu ndani kwetu kuna daladala usiku? Nasikiaga baba anakuambiaga ikisimama panda.''

Juice

Kijana mmoja alitengeneza juice ya mananasi. Alipomaliza kuitengeneza akagundua kuwa maji aliyotumia hakuyachemsha. Akawasha jiko na kuiweka juice yote kwenye sufuria na kuanza kuichemsha.

Monday, July 26, 2010

Ufugaji kisasa

Jamaa mmoja mfugaji aliamua kuwa mfugaji wa kisasa. Hivyo basi akanunua mashine ya kukamulia maziwa ya ng'ombe.

Siku moja mkewe alipotoka akaenda kuijaribu kwa kuchomeka uume wake pale, akaiwasha ikampa matokeo ya kuridhisha.

Alipomaliza akawa anataka kuizima, kila akitafuta hapaoni. Akapiga simu kwa supplier kuomba msaada. ''halo... nimeunua mashine.... ni nzuri sana... je unaichomoaje toka kwenye chuchu za ng'ombe?''

Supplier akamjibu, ''oh, hiyo ipo automatic inajizima baada ya kupata galoni mbili za maziwa.''

Mama kujifungua

Dokta mmoja alipata dharura. Akaenda alipopigiwa simu, kufika akakuta mama mjamzito akikaribia kujifungua.

Hapakuwa na mtu hapo nyumbani zaidi ya huyo mama na mtoto, na umeme ulikatika. Dokta wakati anashughulika kuzalisha akamuomba yule mtoto wa miaka 6 amsaidie kumulika na tochi.

Baada ya mama kujifungua dokta akamuuliza mtoto, ''unasemaje kuhusu mtoto?''
Kale katoto ka miaka 6 kakajibu, ''mfinye akome, aliingia kufanya nini humo?''

Mtoto alipoona

Siku moja mtoto alimuona mama yake akiwa karibu kujifungua. Alipoona nywele akauliza.

Mtoto: Mama, nini hiyo katikati ya miguu yako?
(Akimaanisha nywele)
Mama: (Akamjibu kwa mshangao) ni brush ya kufulia nguo.

Baada ya muda dokta alizinyoa zote.
Mtoto aliporudi akauliza tena, ''brush imeenda wapi mama?''
Mama akajibu, ''nimeipoteza mwanangu.

Siku chache mtoto akamfuata mama yake, ''mama.. mama njoo, nimeiona brush yako anayo house girl anamsafishia baba uso..."

Baada ya shughuli

Mwanaume mmoja baada ya shughuli na mwanamke aliemuopoa, aliangalia mule chumbani kwa yule mwanamke akaona picha. Akauliza:

Mwanaume: Huyu mumeo kwenye picha? (huku akiwa na woga).
Mwanamke: Hapana.
Mwanaume: Je, ni mchumba wako?
Mwanamke: Hapana.
Mwanaume: Sasa ni nani huyu kwenye picha?
Mwanamke: Ni mimi kabla sijafanyiwa upasuaji (operation).

Sunday, July 25, 2010

Duma

Jamaa mmoja alikua anaangalia kipindi cha wanyama. Akamuona Duma (chetah) anamfukuza swala akasema ''khaa, huyu myama ana kiiimbia. Mi akinifukuza wala sikimbii, maana atanikamata tu ya nini nijichoshe wakati kifo kipo palepale.''

Fumanizi

Mwanamke mmoja wakati yupo na kibwana cha nje. Ghafla mumewe akarudi. Hivyo akamua kumpaka unga yule bwana wa nje. Halafu akamwambia agande kama sanamu.

Mume alipoingia akauliza, ''hii sanamu ya uchu umeitoa wapi?'' mke akajibu 'nimeletewa na rafiki yangu.'
Mume akauliza tena, 'mbona naniliu yake kama ina...' (huku akinama kuichungulia)
ndipo jamaa (sanamu akasema) ''oya tuheshmiane''

Maktaba

Dada mmoja alienda maktaba alipofika akamuuliza mhusika pale maktaba 'nimekuja kumuonda daktari.'

Mhusika wa maktaba akajibu huku akimshangaa kimoyo moyo ''dada hapa ni maktaba''
Ndipo yule dada akauliza kwa kunong'ona ''oh, samahani, nimekuja kumuona daktari.''

Nimemfundisha

Mwanamke mmoja akimusimulia shoga yake ''mwenzangu si nimemfundisha mume wangu kuchoma mishkak pale nyumbani chini ya mti?''

Rafiki akauliza, 'kulikoni?'
Manamke akajibu, ''si mishkaki yote inaishia kumpa yule mwanamke upande wa pili.''
Rafiki: Mishkaki ijayo ipakae chroloqin...

Mbele ya kioo

Mwanamke mmoja alimkuta mumewe yupo mbele ya kioo kikubwa akila chakula akiwa hajavaa nguo kabisa.

Mkewe akamuuliza kulikoni? Jamaa akajibu ''naangalia kama napungua, nimepunguza kiwango cha kula''

Malalamiko

Mwanamke: Mume wangu kila nnachompikia anasema sio kizuri.
Rafiki: Umewahi jaribu kitabu cha mapishi?
Mwanamke: Hapana sijajaribu je kinapikwa kwani?

Kasuku wawili

Kasuku wawili kwenye kitabu cha hadithi wakiongea. ''Nimechoka kuishi kwenye hiki kitabu'' mmoja alimwambia mwenzake.

Kasuku mwenzake akamjibu ''mimi nasubiri leo akifika ukurasa nliopo napaa zangu.''

Baba, mama, mtoto

Baba, Mama na mtoto wakiwa mezani wanakula chakula cha jioni. Ndipo mtoto aliponena jambn, ''baba, baba... kitanda chenu kina sifa.''

Baba: Kwanini unasema hivyo mwanangu?
Mtoto: Baba wewe ukisafiri kinapiga kelele usiku kucha.

Mshahara

Jamaa mmoja akimuambia rafiki yake. ''Ndugu yangu... Mimi nadhani mshahara wangu upitie tbl tu moja kwa moja, maana wife ananinyima raha kabsaaa!''