Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Thursday, January 12, 2012

Bar na watu wachache

Jamaa mmoja aliingia bar ilikua ya ndani hivi na watu wachache. Akapita kila meza, kila alipomaliza kuongea neno meza husika walitoka nje. Mpaka akabaki mhudumu wa kaunta tu. Alipomaliza akatoka nje ma kuwaambia warudi ndani.

Walikuta bia zao zote jamaa kanywa, mmoja akatoka mbio na kumfukuza. Kila akijaribu kumuacha jamaa huyu hapa nyuma akauliza "we unanifukuzia nini?" Jamaa akajibu "umekunywa bia yangu niliweka sumu, naitaka."

Ndoa ijayo

Ofisini kulikua hivi:
Mfanyakazi: Boss naomba off kesho nisije nna party ya kumvisha pete mchumba wangu.
Boss: Mwanamke gani chizi atakukubali wewe?
Mfanyakazi: Ni mwanao Jesca boss.

Mgonjwa wa akili

Mgonjwa wa akili alikua akikojoa ghorofani kuelekea chini. Alipomuona nesi akaahirisha. Baadae kumuuliza mbona ulipomuona nesi ui liacha akajibu "angenivuta je si ningeanguka!"

Wednesday, January 11, 2012

Mwizi a.k.a kibaka

Mwizi aliamua kumteka mtoto mmoja wa miaka 10 akikatisha nae sehemu yenye giza nene...
Mtoto: Naogopa...
Mwizi: Sa unafikiri ntakatisha na nani hapa?

Bangi zime...

Jamaa alipiga polisi simu "haloo, jirani yangu ameficha bangi kwenye kuni nyumbani kwake"
Kesho yake polisi walifika na kupekua pamoja na kupasua pasua kuni bila kuona bangi.

Jirani akampigia simu jirani yake "vipi polisi walikuja?" Jamaa akajibu "ndio"
Jirani akaendelea "unaona nlikuambia watakusaidia kupasua kuni, sasa zamu yako wapigie waambie nimefukia cocain kwenye bustani yangu."

Mgojwa hasira

Mgonjwa: Dokta nnasumbuliwa sana na hasira za mara kwa mara hata jambo dogo tu mi ni hasira.
Dokta: Tatizo haswa ni nini?
Mgonjwa: Si nimeshakuambia pumbavu zako unakua kama mwehu bwana.

Kitu msikitini

Msikiti mmoja wakati wa swala ya ijumaa, sheikh alitoa mawaidha muda mrefu saana. Waumini wakaanza ondoka mmoja mmoja.

Mmoja akabaki, sheikh akanena "bora wewe umebaki hao wengine wamekosa heshma"
Muumini akajibu "mi mwenyewe nasubiria mkeka wangu uliokalia."

Mwizi

Jamaa alikua akiandika meseji kwa boss wake akiwa katika daladala kuwa atachelewa kidogo kazini. Ghafla alipomaliza kuandika mwizi akaikwapua jamaa badala ya kuita mwizi... Mwizii akamuambia "bonyeza send, bonyeza send..."

Unyumba

Mwanamke akiwa mbele ya wazazi wake, yaani,wakwe wa mumewe.
Mwanamke: Wazazi wangu nimewaita mume wangu hanipi unyumba kabisa wiki sasa.
Mzazi: Mkwe wetu haya tuambie nini shida?
Mume: Dokta kaniambia nisipendelee vitu vitamu kwa sababu nna kisukari.

Kila kitu kikubwa

Kipofu aliagiza bia wakamletea kwenye jagi kubwa. Akanena "hee mbona kubwa hivi?"

Wa pembeni akajibu "Dar kila kitu kikubwa"
Kipofu akaomba kwenda chooni, akaingie mlango wa pili kushoto.

Kipofu akaingia mlango wa 3.
...akatumbukia kwenye bwawa la kuogelea akijua katumbukia kwenye choo akawa anapayuka kwa sauti "usiflash... Usiflash..."

Tuesday, January 10, 2012

Taxi driver mpya

Abiria kwenye taxi siti alimgusa bega dereva, alistuka mpaka kugonga ukuta wa watu.
Dereva: Dah kaka usifanye hivyo tena.
Abiria: Hamna shida nilikua nakuita tu.
Dereva: Ndio, leo ndio nimeanza hii kazi ya taxi kabla ya hapo nikiendesha gari la kubeba maiti.

Mteka nyara

Njaa ilimbana jamaa akaamua kumteka nyara mtoto wa miaka 6. Akamuandikia kikaratasi kimeandikwa hivi:
"nimemteka mwanao, anakuja kukupatia hiki kikaratasi na kesho uweke milioni 10 kwenye kona pale jalalani"

Mwenye mtoto nae akaandika kikaratasi na kumtuma mtoto kimeandikwa hivi:
"Kivo huu si mwandiko wako asa inakuwaje unamteka mwanangu?"

Maandazi 6

Mwalimu: Joseph nikikupa maandazi 6 nkatoa mawili yatabaki mangapi?
Joseph: Kama ukinipa na mchuzi halibaki hata moja.

Monday, January 9, 2012

Nyoka na panya

Nyoka: Oya vipi mbona unaniangalia sana?
Panya: Mbona unajistukia?
Nyoka: Muone ndo maana una ndevu...
Panya: Bora mie, we kubwa zima watambaa hadi leo.

Sunday, January 8, 2012

Darasa la hisabati

Mama: Mbona umenuna mwanangu?
Mtoto: Mwalimu wa hesabu hajaja leo.
Mama akajua mwanae kichwa kwenye hesabu na kupenda.
Mama: Usijali mwanangu ntamuambia aje kukufundisha hapa hapa nyumbani.
Mtoto: Tatizo yeye pekee ndio anauza ubuyu ndio maana.

Sumu ya panya

Jamaa aliwategea sumu ya panya kwwnye nyama ya nguruwe nyumbani kwake. Asubuhi alipoamka akakuta kikaratasi kimeandikwa "hatuli nguruwe, we samaki kesho uone."

Utambulisho

Walipofika mbeya kikazi wakati wa kujitambulisha.
Wa mimi naitwa Mwakasitu.
Wa pili: Mimi naitwa Mwakasege.
Wa tatu anaitwa Juma nae akanena "mimi naitwa Mwajuma"

Friday, January 6, 2012

Ombaomba

Mwanamke alikaa kwenye viti vya bustani za katikati ya mji. Punde akaja ombaomba wa kiume.

Ombaomba: Oh mpenzi umekuja tu-enjoy.
Mwanamke: {kwa hasira} We umechanganyikiwa...!!?
Ombaomba: Sasa unafanya nini kitandani kwangu.

Mkojo ulibana

Jamaa alibanwa mkojo, akawa mbio mbio anakimbilia chooni kukojoa. Bahati mbaya akajikojolea njiani. Akaamua kurudi kwenye mkutano ivo ivo kwa vile ameshakojoa.

Majambazi

Majambazi waliingia benk kuiba, baada ya kubeba fedha za kutosha wakati wanaindoka mmoja wa majambazi waliovaa mpaka usoni; alimuandikia namba mrembo mmoja wa pale kauta namba ya simu vile amemzimikia.

Mchina kaibiwa

Mchina alipigwa mtama na kibaka akaibiwa simu. Mchina akaanza mfukuza kibaka, kibaka akaona isiwe tabu akaidondosha simu. Mchina akaiokota na kuendelea mfukuza.

Kibaka "we si nimekupa simu yako?"
Mchina akajibu "ndio umenipa bado mtama"

Tuesday, January 3, 2012

Mapacha

Mke alizaa mapacha, mume alipofika hosp. Akamuuliza mkewe "huyu mtoto m1 wangu na huyu mwingine utanieleza vizuri wa nani?"

Ndoa ikifungwa

Padre akiuliza umati kabla ya kufungisha ndoa kanisani "kuna yeyote mwenye kipingamizi ndoa hii isifungwe?"

Sauti ikasikika nyuma "padre subiri kidogo." Kisha jamaa akasogea mbele mbele.
Padre: Je, unapingamizi lolote ndugu?
Jamaa: Hapana kule nyuma nlikua sikusikii vizuri.

Maiti ikioshwa

Maiti ilikua inaoshwa, ngafla ikaanza kucheka waoshaji wakauliza "hii maiti inacheka nini?"
Maiti ikajibu "mnanitekenya bwana alahh!"

Mapadre na vekeshen

Ma-padre wawili walenda mbali kidogo kula starehe (bata). Ili wasijulikane wakanunua nguo na kupiga swaga za mtaani. Punde akapita dada mmoja wakammezea mate, dada akawasalimia "fatha mambo?"

Wasijue kawajuaje... Siku ya pili na ya tatu ivo ivo wakamuuliza: "we umetutambuaje...?"
Dada akajibu: Mi si Sister Rosa umenisahau?

Monday, January 2, 2012

Condom

Vijana wawili walienda mbiombio kwa dokta:
Kijana: Dokta nimemeza condom bahati mbaya nisaidie kuitoa.
Dokta: Huyu uliekuja nae yeye ni nani yako?
Kijana: Rafiki yangu ndio mwenye condom yake.

Nzuri na mbaya

Dokta: Mzee nna habari mbaya na nzuri, nianze ipi?
Mzee: Anza na mbaya ifuate nzuri.
Dokta: Mbaya mguu wako tumeukata kabisa. Na nzuri nitakununulia kiatu kwa bei rahisi tu.

Sunday, January 1, 2012

Alipobanwa mtihani

Mwanafunzi alibambwa kwenye mtihani:
Mwalimu: Uliiua unampigia simu nani akupe majibu?
Mwanafunzi: Mwalimu ile haikua cheating mtu nliempigia hajui jibu pia.

Jaza fomu

Jamaa mmoja alipokwama kujaza kwenye fomu.
Jamaa: Samahani sikumbuki jina la hospitali nlilozaliwa.
Mhudumu: Si lazima hospitali jaza mji uliozaliwa tu.
Jamaa: Nimejaza Kitandani, ndii sehemu nlipozaliwa.

Mwaka Mpya.

Heri ya Mwaka Mpya kwa wanablog hii wote.
Mwenyezi Mungu ashukuriwe.