Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Tuesday, August 17, 2010

Simu kwenye basi

Mtoto mmoja wa makamo siku moja mama yake alimnunulia chupi inafanana kabisa na baba yake.
Sasa siku moja wakati yupo kwenye daladala na mama yake mara simu ikaita ya mama yake.

Mama kabla hajaipokea akamuambia mwanae ''baba huyo anapiga simu''
yule mtoto kabla hata mama yake hajaipokoea kwa sauti ya kusikika mote kwenye daladala akasema ''mama kisha muulize kama amejisahau amevaa chupi yangu, mie sijaiona leo.''

Kijiti

Jamaa alipomaliza pata mlo kwenye retaurant moja na mrembo wake akamuuliza mrembo wake hivi ''nikuagizie toothpick?''
Yule mrembo akamjibu huku akiona ona aibu ''enhe! Asante nimeshiba sana''

Mwalimu darasani

Mtoto mmoja alimuuliza mama yake...
''mama, kwani mwalimu haruhusiwi kuvaa chupi?''
Mama kwa shauku na mshangao akauliza ''...mh! kulikoni mwanangu umesikia wapi hiyo?...''

Mtoto akajibu ''mi nashangaa mama, labda atakua anasahau... Si mwalimu wetu wa darasa ndio havaagi''
Mama akauliza ''we umejuaje?''

Mtoto: Si namtegesheaga kioo chini ya miguu yake.

Viatu vya ngozi

Mtoto mmoja alikutywa na mama yake akiwa na viatu vya ngozi... Mama yake akamuuliza ''Jasmine mbona umekaa chini?''

Jasmine akajibu ''ninaviandaa viatu vyangu''
Mama: Ooh umekua mtoto mzuri siku hizi unajua mpaka kupaka kiwi viatu? Wow!
Jasmine: Mama!! Nikipaka kiwi viatu si vitaharibika?

Mama akajibu ''haapaana mwanangu kwani vipi?''
Jasmine: Me mevipaka losheni kwani si vya ngozi na vyenyewe? Kiwi itaharibuu...

Swaumu

Jamaa alimuona mwenzake ni kama anatafuta kitu alichokipoteza akamuuliza ''mwenzangu vipi mbona kama hueleweki umepoteza kitu nini?''

Ndipo jamaa akamjibu ''ndio, nimeshangaa njaa imeacha kuuma ghafla nlipofika maeneo haya, hivyo laziima ntakua nimeidondosha hapa swaumu yangu''

Babashop

Mahause girl wameenda town wakawa wanaona kila salon imeandikwa barber shop. Wakatiaje, huyo baba shop tajiri ana maduka mji mzima.

Monday, August 16, 2010

Uwanjani

Siku moja wakati tupo uwanjani twacheza mpira wa kikapu, jamaa yetu mmoja ana maneno mengi sana.

Moja kati ya wachezaji akapewa pasi ikamponyoka mikononi... Yule maneno mengi akasema kwa sauti ''wee viiipi weewe unashindwa daka mpira? Unaogea kopo nini?''

Siku moja nyingine akaja uwanjani akiwa amevaa fulana nyeupe, mwisho wa siku baada ya kucheza kikapu akagundua fulana yake imechafuka maeneo ya mabegani akauliza kwa sauti ''nani kanikanyaga jamani?''

Moto

Jamaa mmoja alipoingia nyumba moja na kuona moto kwa ajili ya kutoa joto sebuleni (fire place).
Akaanza kwa kusema ''moto moto... moto..." huku akitafuta ndoo ya maji akauzime.

Lift

Jamaa mmoja aliomba lifti, ikawa hivi:

Jamaa: Naomba lift ndugu yangu.
Dereva: Utapakia wapi sasa ndugu yangu?
Jamaa: Hata hapo mbele.
Dereva: Hapa mbele hairuhusiwi abiria.

Jamaa: Basi hata huku nyuma.
Dereva: We huoni kama hili ni karandinga (lori la kubebea mahabusu/wafungwa).
Jamaa: Sasa mbona hao jamaa nyuma umewapa lift (wafungwa/mahabusu)?

Sunday, August 15, 2010

Kumtembelea mchumba

Kijana mmoja alienda mtembelea msichana wake anaesoma nae chuo kimoja. Jamaa alipofika nyumba husika akawa anataka kuishia nje, mzee mwenye nyumba akamsihi mtoto wake huyo mgeni aingie tu ndani.

Jamaa alipoingia si akakuta mzee anasafisha bunduki huku akiongea ''kijana... mambo ya shule huko huko shule... mmemaliza assignment zenu?''

Nyoka

''Dokta nadhani nna matatizo ya kuona siku hizi'' nyoka akimuambia daktari.
Daktari akamuambia ''ntakusaidia.''

Baada ya siku kadhaa nyoka akarudi tena, dokta akamuuliza ''vipi ile miwani niliyokupatia haijakusaidia?''

Nyoka akajibu ''dokta nimegundua kuwa kumbe kwa muda wa miaka mitatu nilikuwa nikiishi chini ya maji''

Mugongo mugongo

Baba mmoja na mama wakati wanajiandaa kufanya mapenzi mtoto wao mdogo wa miaka miwili na nusu aka-a-mka ''baba na mimi naomba nipande mgongonu'' mtoto aliomba.

Baba akawa anakataa, mama akasema ''muache tu hamna shida'' basi mtoto akapanda.
Wakati wanashughulika mama akawa amezidiwa na utamu kweli kweli mtoto akasema ''baba jishikilia jana kidogo tuanguke wakati wakati nimepanda mgongoni mwa yule mleta maziwa''

Saturday, August 14, 2010

Msibani

Mtoto mmoja alishuhudia kwa mara ya kwanza msiba mtu akizikwa akamuuliza mama yake ''mama... mama... Sasa nani atakua anambadilisha nguo huyo mtu wanaemfukia kwenye sanduku la mbao? Si zitachafuka haraka?''

Nguo ya mapenzi

Mwanamke mmoja alikuwa uchi wa nyama bibi yake akamuuliza pale sebuleni, ''mbona hivyo kulikoni?''
Mwanamke akajibu ''hii ni nguo ya mapenzi namsubiri muwe wangu.''

Baadae mume aliporudi akamkuta bibi yake mkewe nae hajavaa nguo ''bibi vipi leo una nini?"
Bibi akajibu, ''nimevaa nguo ya mapenzi namsubiri babu yenu''

Mume wa yule mwanamke akamjibu ''oh kumbe, sasa mbona hujainyoosha na pasi?"
(makunyanzi mwilini)

Biashara

Kaka mmoja akiitangaza biashara yake mbele ya mteja, ''kaka nauza vyombo vya plastic, vya udongo na miswaki used''

Kuchimba dawa

Mtoto mmoja alikuwa na anko ake wakitoka kijiji kimoja kwenda kingine, mara yule mtoto akabanwa na haja kubwa akamuomba anko yake amsubiri aingie kuchimba dawa.

Wakati yupo upande wa pili wa kichaka akamuuliza anko yake ''anko nachimba shimo kabla au baada?''

Friday, August 13, 2010

Mwalimu wa biology

Mwalimu mmoja wa baiolijia akifundisha darasani lile somo la viungo vya uzazi, akauliza "Kuna ambae hajaelewa mpaka nilipofikia sasa?"
Mwanafunzi mmoja akanyoosha kidole na kuuliza "Mwalimu mi umeniacha kidogo, labda ungevua suruali ukatuonyesha ndio tutaelewa vyema kwa mifano hai"

Bwenini

Mkufunzi mmoja wa chuo akiwaambia wanafunzi wa mwaka wa kwanza masharti "Bweni la wanaume ni la wanaume tu na la wanawake ni la wanawake tu" huku akiendelea kuongea "ukifumwa mara ya kwanza utalipa faini ya shilingi elfu 20, mara ya pili elfu 60, mara ya tatu laki mona na 80"

Mwanafunzi mmoja akauliza "Je kwa semester (Muhula) nzima ni shilingi ngapi?"

Wakili na Daktari

Mzee mmoja alipoona ana masaa 24 kabla hajafa pale hospitali. Akaagiza dokta na Mwanasheria wake waje.

Dokta akauliza ''hapa nafanya nini?'' mzee akajibu ''nothing, we simama tu hapo hapo.''

Mwanasheria nae akauliza ''hapa nafanya nini?'' mzee akajibu ''nothing, we simama tu hapo hapo.''

Baadae wakauliza tena pale waliposimama mzee akawajibu ''Kristo alikufa na wezi wawili, so na mimi nafanya vivyo hivyo''

Kuachana

Mwanamke mmoja alipovunja ukimya akamuambia mpenzi wake waachane. Mpenzi wake kwa vile alikuwa mji mwingine kabisa, akatuma picha 13 na kumuambia ''sikumbuki vizuri we ni yupi, chukua picha yako zingine nirudishie''

Thursday, August 12, 2010

Kabla ya kufa

Mume: Mke wangu nikifa utaolewa tena?
Mke: Ndio, itategemea.
Mume: Utampa gari yangu aendeshe.
Mke: Mh! Nadhani.
Mume: Utamuacha akae kwenye kiti changu sebuleni?
Mke: Labda.
Mume: Utamuacha avae suti yangu nzuri?
Mke: No, ye ni mfupi.

Wodini

Jamaa mmoja aliamka akiwa kitandani wodini baada ya kupata ajali mbaya. Akauliza ''dokta... dokta... Mbona siusikii kabisa mkono wangu wala mguu..."

Dokta akajibu, 'huwezi isikia kwa sababu nimeikata yote'

Huzurio kwa dokta

Mwanamke mmoja alienda kwa dokta kufanya check-up. Kwa vile alikuwa anaona aibu akamuambia dokta azime taa ili avue nguo. Alipomaliza akamuuliza ''dokta niweke wapi nguo zangu?''

Dokta akajibu ''weka kwa hapa karibu na zangu''

Ajali-pikipiki

Dereva mmoja wa pikipiki alivaa koti nyuma mbele, akapata ajali.

Wasamaria walipokuja kumsaidia wakajua shingo imegeuka wakaanza kuigeuza kugeukia usawa wa koti. Kumbe ndio kifo.

Wednesday, August 11, 2010

Kuibiwa

Mzee mmoja na mkewe wakati wanatoka supermarket na mkewe walikuta gari yao haipo walipoipaki. Wakaenda polisi kutoa taharifa.
Polisi akashauri waje nae sehemu ya tukia kutafuta ushahidi.

Wakalikuta gari lao limerudi na kuna kibahasha kimewekwa kwenye wiper kimeandikwa hivi ''samahani nilichukua gari lako, mke wangu alishikwa na uchungu nkaamua kumkimbiza hospitalini. Pole kwa usumbufu. Chukua tiketi mbili hizo mje kwenye tamasha kama zawadi yangu''

Siku walipoenda kwenye tamasha kurudi wakakuta nyumba imeibiwa vile vitu vya thamani vyooote na kukuta barua imeandikwa ''nina shida ya ada ya mwanangu hivyo nimekuja tena.....''

Maji ya kunywa

Jamaa mmoja aliomba majiya kunywa, alipopewa akanywa. Alipomaliza akauliza maji yako matamu kweli ya umeyahifadhi kwenye mtungi nini?

Mwenyeji wake akajibu, ''hapana atii, haya ya mferejini''
Jamaa akashtuka ''mferejini?''
Yule jamaa akamjibu ''yakhe si bomba la maji kule Zanzibar twaita mfereji atii.
Ndipo jamaa akasema ''aanhaa kumbe, duh!''

Ajali

Mtoto mmoja alimuambia mama yake alipopigiwa simu: ''hujambo mwanangu?''
Mtoto akajibu ''sijambo mama ila nimepata ajali, na polisi wananifukuza hivi nnavyoongea''

Mama akashtuka na kumuuliza vizuri, ''eenh!! Unasema??''
Mtoto akaendelea kujibu, ''ndio hapa nyumbani kwenye video game''

Tuesday, August 10, 2010

Ndoto isiyoeleweka

Jamaa: Dokta nna tatizo, nikilala nasikia kitu uvunguni mwa kitanda. Nikichungulia nasikia juu ya kitanda.
Dokta: Noo mara mbili kwa wiki ofisini kwangu ntakusaidia kulitatua.

Jamaa: Itakuwa shingapi kwa kila nikija?
Dokta: Itakuwa elfu 30 tu.

siku chache baadae walipokutana mtaani.
Dokta: Mbona hukuja tena?
Jamaa: Nilipata mtu alinisaidia kumaliza tatizo lile.
Dokta: Alikusaidiaje sasa?
Jamaa: Aling'oa miguu yote ya kitanda kwa shilingi elfu 10 tu.

Monday, August 9, 2010

Nyama ya mbuzi

Kwenye sherehe ndogo nyumba fulani waliandaa party. Mzee mwenye nyumba akaagiza wachinje mbuzi.

Mwisho wa siku aliporudi nyumbani alipopita zizini akaona jambo... Akaanza kubwata alipoingia sebuleni, ''...mmeniudhi sana... Mi mesema mchinje mbuzi mmoja mmechinja wawili..." alifoka akafoka.

Mke: Mume wangu jamani ni mbuzi mmoja tu kachinjwa...
Mume: HAPANA SI KWELI...
Mke: Si kweli kivipi?
Mume: Si mmemchinja yule mbuzi wangu mjamzito...

Ajali na msaada

Gari moja lilipata ajali, mwanamke mmoja akawa wa kwanza kufika kutoa msaada.
Hata kabla hajaanza akatokea jamaa na kumsukuma yule mwanamke na kusema "pisha dada, nimesomea kutoa first aid.''

Yule mwanamke baada kama ya dakika 3 nae akanena ''ukifika muda wa kumuhitaji daktari nipo hapa''