Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Monday, August 16, 2010

Uwanjani

Siku moja wakati tupo uwanjani twacheza mpira wa kikapu, jamaa yetu mmoja ana maneno mengi sana.

Moja kati ya wachezaji akapewa pasi ikamponyoka mikononi... Yule maneno mengi akasema kwa sauti ''wee viiipi weewe unashindwa daka mpira? Unaogea kopo nini?''

Siku moja nyingine akaja uwanjani akiwa amevaa fulana nyeupe, mwisho wa siku baada ya kucheza kikapu akagundua fulana yake imechafuka maeneo ya mabegani akauliza kwa sauti ''nani kanikanyaga jamani?''

No comments:

Post a Comment