Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Wednesday, August 11, 2010

Kuibiwa

Mzee mmoja na mkewe wakati wanatoka supermarket na mkewe walikuta gari yao haipo walipoipaki. Wakaenda polisi kutoa taharifa.
Polisi akashauri waje nae sehemu ya tukia kutafuta ushahidi.

Wakalikuta gari lao limerudi na kuna kibahasha kimewekwa kwenye wiper kimeandikwa hivi ''samahani nilichukua gari lako, mke wangu alishikwa na uchungu nkaamua kumkimbiza hospitalini. Pole kwa usumbufu. Chukua tiketi mbili hizo mje kwenye tamasha kama zawadi yangu''

Siku walipoenda kwenye tamasha kurudi wakakuta nyumba imeibiwa vile vitu vya thamani vyooote na kukuta barua imeandikwa ''nina shida ya ada ya mwanangu hivyo nimekuja tena.....''

No comments:

Post a Comment