Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Tuesday, August 3, 2010

Ahera

Jamaa alikufa akaenda ahera, huko akakutana na shetani, akamuambia "huku kuna vyumba vitatu, unatakiwa kuchagua kimoja ndio kitakuwa unaishi humo"
Jamaa akakubali na kwenda:

Chumba cha kwanza: Akakuta watu wamelala juu ya kitanda cha miba. Akasema "hapana ngoja niangalia chumba kingine"
Chumba cha pili: Akakuta watu wanaogelea kwenye maji machafu. Jamaa akakataa tena.
Chumba cha tatu: Akakuta watu wamekaa wanapata kahawa. Akasema "hiki ndio kinanifaa" akaingia.

Baada ya dakika chache akaja mtu na kuwa tangazia "haya mapumziko ya kahawa yameisha "kila mtu arudi kwenye kiti chake nyoka mmoja mmoja anapita kuwagonga"

No comments:

Post a Comment