Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Sunday, August 8, 2010

Bar

Jamaa mmoja aliingia bar moja uko majuu. Alipofika akaagiza pale kaunta kichwaji kwenye glasi ndogo akanywa.

Alipomaliza akaambiwa bei yake ni sarafu (coin).
Kwa vile kaunta ni kubwa akaipiga na kidole sarafu moja mpaka mwisho wa kaunta upande wa kushoto, na nyingine upande wa kulia na ya mwisho akaiweka katikati ya kaunta (viti virefu). Kisha akatimua.

Mhudumu akamuangaliaa asijue la kumfanya.

Siku ya pili jamaa akaja tena akafanya vile vie.
Siku ya tatu pia... Akatoa noti wakati wa malipo na chenji inatakiwa zirudi Sarafu mbili.

Mhudumu akachukua sarafu ya kwanza akaiweka mwisho kabisa mwa kauta kushoto na ingine kulia. Ili tu ampe huyo jamaa usumbufu aliompatia siku mbili zilizopita.

Yule mteja alipoona vile akato sarafu na kuiweka katikati ya kaunta na kumuambia ''nipe glasi nyingine.''

No comments:

Post a Comment