Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Monday, August 9, 2010

Kwa mshauri

Mume na mke walienda kwa mshauri kuhusiana na matatizo ya ndoa yao. Walipofika, mwanamke akaanza elezea kwa muda wa dakika 15 kuhusu kero azipatazo.

Alipomaliza, mshauri akanyanyuka kwenye kiti akaenda akamshika yule mwanamke kwa kuonye anamjali, akambusu hapa na pale. Yule mwanamke akabaki kimya bila la kuongea.

Mume akauliza, ''umewezaje kumnyamazisha?''
Mshauri akajibu "unatakiwa umfanyie hivyo kila siku."
Mume akajibu "basi ntakua namleta kwako"

No comments:

Post a Comment