Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Friday, August 6, 2010

Ajali

Marafiki wawili wa kiume walipata ajali, bahati nzuri hawakuumia kama ilivyo kwa gari.

Mmoja akamuambia mwenzake, ''kabla hatujalaumiana kosa la nani ngoja tushereke tumepona''
Mwenzake akajibu, ''kweli kabisa tufanye hivyo.''

Wakachukua chupa ya pombe kali kwenye gari haikuvunjika wa kwanza akanywa kisha akaifuta chupa na kumpa mwenzake nae anywe.."

Mwenzake akamjibu ''hapana ngoja kwanza mpaka trafiki polisi aje...''

No comments:

Post a Comment