Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Tuesday, June 22, 2010

Fundi bomba

Mtoto mmoja alikutana na ka_rafiki kake na kuambiwa na huyo rafiki yake "unajua watu wazima wana siri wote?" kale katoto kakajibu "kweli?"
Mwenzake akamwambia nenda kajaribu kama watu watatu kesho uje na jibu...

Mtoto alipofika kwao akamfuata mama yake na kumuambia "najua ukweli wote" mama akatoa elfu tano akampa na kumuambia "usimuambie baba yako"

Mtoto aliporudi baba yake akamfuata na kumuambia "najua ukweli wote" baba akatoa elfu kumi akampa na kumuambia "usimuambie mama yako."

Asubuhi mtoto akamfuata fundi bomba na kumuambia "najua ukweli wote" yule fundi bomba akasimama na kumuambia "oooh, vizuri. Njoo umkumbatie baba yako mzazi"

No comments:

Post a Comment