Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Monday, June 21, 2010

Kufukuzwa na polisi

Kibaka mmoja alikuwa anafukuzwa na polisi gizani vichochoroni. Ngoma ikawa hivi, kila akigeuka nyuma polisi wapo nae. Akaona eeh! Isiwe shida.

Akafika sehemu akainama akaitanua fensi ya nyaya mbili (yaani kaishika kwa mikono mmoja katanua kwenda juu na wa pili kwenda chini) halafu akapenya mguu mmoja baada ya mwingine.

Kisha akairudishia ile fensi kama alivyoitanua kiasha akaanza mbio tena (hiyo ni kitendo cha sekunde chache mno)

Wale polisi waliiona picha yote walipofika pale eneo la tukio wakapunguza mwendo huku wakipapasa gizani labda wataigusa hiyo fensi isijewajeruhi kumbe hapakuwa na fensi wala nini...

No comments:

Post a Comment