Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Wednesday, June 23, 2010

Vichaa

Wagonjwa wa akili wawili walikuwa pembeni mwa bwawa la kuogelea. Mmoja akaingia, yule wa pili akaingia na yeye kumuokoa mwenzake.

Baadae daktari akamuambia yule wa pili ''hongera sana umefanikiwa muokoa mwenzako, tutakuachia huru umepona sasa''
yule wa pili alifurahi sana.

Daktari akaendelea: ila bahati mbaya mwenzako kajinyonga tumemkuta. Yule kichaa wa pili akajibu ''oh, hapo nilimuweka mimi ili akauke''

No comments:

Post a Comment