Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Saturday, June 26, 2010

Simu hospitali

Mwanaume mmoja alipiga simu hospitali ya wagonjwa wa akili akapokea mtu wa mapokezi na kumuambia, ''kuna mgonjwa yeyote chumba namba 30?''

Mtu wa mapokezi akaenda kuangalia na kurudi akamjibu yule mtu kwenye simu ''hamna mtu kwenye hicho chumba.''

Jamaa kwenye simu akaongea... ''oh! hiyo inamaanisha nimefanikiwa kutoroka.''

No comments:

Post a Comment