Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Monday, June 14, 2010

Mke na mume

Jamaa mmoja alienda kupata ushauri kwa daktari baada ya kuhisi kama mkewe hasikii vyema (dalili za ukiziwi). Dokta akamuambia ukirudi nyumbani wakati anapika simama hatua 15 nyuma yake na muulize kama hasikii sogea mbele kidogo vivyo hivyo na uliza swali hilo hilo.

Aliporudi home akakuta mkewe anapika, akasimama hatua 15 nyuma na kumuuliza ''mke wangu leo unapika chakula gani cha jioni?''

Hakupata majibu, akasogea kidogo mke hakusikia tena, akasogea tena hakupata jibu tena, mwisho akamsogelea kabisa na kumuuliza tena ''mke wangu leo unapika chakula gani cha jioni?''

Mke akamjibu, ''kwa mara ya nne najibu, nimesema Kuku''

*cheka unenepe*

No comments:

Post a Comment