Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Friday, June 18, 2010

Ushabiki kombe la dunia...

Jamaa mmoja alikuwa na tiketi mbili za kombe la dunia.

Alipofika uwanjani jamaa mwingine akaja na kuomba kukaa ile siti isiyo na mtu pembeni yake. Kisha maongezi yakaendelea.

Aliyetoa siti: Hii siti ilikuwa ya mke wangu, ila bahati mbaya amefariki.

Aliyepewa siti: Ooh, pole sana, sasa si ungempa ndugu yeyote akaja kuangalia mpira badala yake?

Aliyetoa siti: Wote wameenda kwenye mazishi...

1 comment: