Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Sunday, June 13, 2010

WorldCup

Mume alipokuwa anaangalia mpira maongezi yao na mkewe yakawa hivi:
Mke: Mume wangu njoo itengeneze hii taa ya jikoni.
Mume: Now? I don't think so.
Mke: basi njoo uurekebishe huu mlango...
Mume: I don't think so.
Mke: Basi pale kwenye sinki panaleta shida.
Mume: Not now.
Mume akaona kero akaondoka kwenda kuangalizia mpira Bar. Wakati yupo huko akajiona amefanya sivyo ndivyo akaanza kurudi nyumbani.
Akakuta kila alichoambiwa kimetengenezwa. Akauliza:

Mume: Imekuwaje hivi vitu vyote vimetengenezwa?
Mke: Alikuja kijana mmoja akanikuta nje hapo nalia ndipo akaamua kunipa msaada, na sikuwa na cha kumpa zaidi ya ile TV set yetu.

No comments:

Post a Comment